7 Desemba 2015 - 17:30
Majeshi ya Syria yazidi kusonga mbele katika mikoa mitatu (Halab, Lattikia na Damacuas)

Majeshi ya Syria katika mwendelezo wake wa kufanya mashambulizi katika mikoa mitatu ya Damascus, Halab na Lattikia, nakufanikiwa kuikomboa mija kadha katika mikoa hiyo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Syria yakishirkiana na majeshi ya kujitolea ya wanachi leo wamefanikiwa kusonga mbele katika mwendelezo wa mashambulio yake katika mikoa hiyo mitatu nchini humo.
Kwamujibu wa Televishen ya Almayadin kuhusu mashambulio hayo imetangaza kuwa majeshi ya Syria yamefanikiwa kuikomboa miji kadhaa katika mikoa mitatu nchini humo.
Kwa mujibu wa habari hii majeshi ya Syria yameweza kuukomboa mji wa (Alhamra, Halsah, Zaitun na Alqalajia) katika mkoa wa Halab kutoka mikononi mwa magaidi na kuwasababishia maafa makubwa magaidi hao.
Aidha jeshi la Syria limewateka  magaidi watano kutoka katika kikundi cha “ Jabhatu Nusra na Jaishul Fathi” baada ya kuiteka wilaya ya Halsah, hivyo basi majeshi ya Syria katika mwendelezo wa mashambulio hayo wamewateka magaidi wengi wakiwa ni wananchi wa mataifa mbalimbali duniani.
Kwa upande wa mkoa wa Lattikia kadhalika jeshi hilo likishirikia na majeshi yakujitolea wananchi wamefanikiwa kuikomboa miji miwili ya “akuu na Buzul Hatab” mkoani humo.
Kadhalika jeshi hilo limefanya mashambulizi makali katika mjumuiko wa miinuko muhimu ya “Sahlul Alaab” ambayo ipo baina ya mkoa wa Lattikia na Adlib na kuukomboa mjumuiko wa milima hiyo muhimu iliopo mashariki mwa Sahlul Alaab.
Pia katika mkoa wa Damascus majeshi ya Syria yameweza kusonga mbele kwa kiasi kikubwa kuelekea uanja wa ndege wa Al Hityati uliopo katika mkoa huo muhimu.

mwisho wa Habari/290